Monday, February 8, 2021

🍃💟JINSI YA KUPIKA SKONZI LAINI🍃*



*🍃💟Vipimo🍃*
 
🍃Unga -  4 Vikombe vya chai
 

🍃Sukari -  4 vijiko vya chakula

 
🍃Chumvi - 1 Kijiko cha chai

 
🍃Hamira - 1 Kijiko cha chakula

 🍃Siagi -  ¼ Kikombe cha chai

 
🍃Maziwa -  1 ½ Vikombe vha chai
 
Yai -  1 Moja
 
Ufuta - Kiasi ya kunyunyizia juu

 
*🍃💟Namna Ya Kutayarisha Na Kupika🍃*

🍃Katika bakuli changanya vipimo vyote isipikuwa ufuta.

🍃Kisha ukande unga huku unanyunyizia unga ukiwa unashika.

🍃Funika mchanganyiko na weka pahali penye joto hadi iimuke.
Halafu fanya viduara na viweke kwenye treya ya kuchomea iliyopakwa siagi.

🍃Ziache pahali penye joto hadi zimuuke kwa mara ya pili.

🍃Washa oveni moto wa 350°.

Pakiza (brush) Yai uliopiga au maziwa juu ya vile vidonge kisha nyunyizia ufuta juu.

🍃Kisha vumbika kwenye oveni kwa muda wa dakika 15  hiv au kama unatumia jiko la mkaa palia kama upaliavyo wali chini acha moto  kidogo na juu weka mfuniko wenye makaa ya moto na kaa dakika 20 hivi kisha chungulia kama zimekua za brown na kugeuka rangi  zitakuwa tayari kuliwa.

*TAMU:* 👌


No comments:

Post a Comment