Monday, February 8, 2021

*ROSTI LA NYAMA YA NG'OMBE*





         *MAHITAJI*


✓ Nyama Nusu (Tumia Nyama kiasi Unachopenda) 

✓ Nyanya *3* kubwa/Kiasi unachopenda

✓ Tomato paste kijiko *1*

✓ Kitunguu/swaumu kijiko  *1*

✓ Hoho  *1 - 2* /Kiasi Unachopenda 

✓ Karoti  *1 - 2* /Kiasi  unachopenda

✓ Pilipili ya Unga (Sio lazima) 

✓ Mafuta ya kupikia kiasi 


       *JINSI YA KUPIKA ROSTI  LAKO*


➖Chemsha nyama adi iive
 Weka sufulia jikon weka mafuta ya kupikia kiasi
 
➖ Halafu Weka kitunguu swaumu, tia nyama koroga Kwa pamoja than wacha nyama yako ipwage vizuri 

➖ Halafu Geuza Nyama yako  weka tomato paste koroga Kwa pamoja 

➖ Baada ya dakika kadhaa geuza Nyama yako  Weka nyanya zako  funika adi ziive halafu tia hoho na karoti na pili pili koroga vizuri iwache Nyama yako iive vizuri 

➖Halafu  weka mchuzi/Kiasi cha Maji  unachotaka,  weka na chumvi kiasi funika iwache  ipwage Kwa dakika kadhaa

➖Baada ya Muda Epua ROSTI lako na IPO tayar Kwa Kuliwa 

➖Unaweza Kutumia ROSTI yako Kwa Kula na Wali, Pilau, Biriani ,  Mandazi, MIKATE, n.k

No comments:

Post a Comment