Thursday, February 4, 2021

JINSI YA KUPIKA WALI WA RANGI TATU*




*MAHITAJI*


*WALI WA MANJANO*

1- Mchele wa basmati kikombe 1 cha chai.

2- Mafuta ya kupikia kijiko1 ½.

3_Nyanya 2 zilizomenywa na kukatwakatwa.

4_ Karoti 3 zilizochemshwa na kuiva.

5- Unga wa binzari 1/4 kijiko.

6_Chumvi kiasi.

7- Kwa wali wa mweupe.

8_ Mchele wa basmati kikombe 1 cha chai.

9_ Mafuta ya kupikia kijiko1 ½.

10_ Tui la nazi kikombe 1.

11_ Unga wa hiliki Kijiko 11/2 chachai.


*WALI WA KIJANI*


*MAHITAJI*

1- Mchele wa basmati kikombe 1 cha chai.

2- Mafuta ya kupikia kijiko 1 ½.

3- Chumvi kiasi.

4- Vitunguu maji 2.

5- Kitunguu saumu kilichopondwa 1.

6- Tangawizi iliyopondwa 1.

7- Nazi iliyosagwa vijiko 2.

8- Majani 8 hadi 10 ya mnanaa.

9- Majani ya giligilani kikombe kimoja.

10- Pilipili manga kijiko 1.

11- Garam masala kijiko 1 cha chai.

12- Namna ya kuandaa.

13- Unatakiwa kupika wali wako katika sufuria tatu tofauti. Kwa.



*WALI MWEUPE*

1- Wali mweupe unatakiwa kupika kama ilivyozoeleka huku ukiongeza hiliki kama kiungo chako.

2- Unachotakiwa kufanya ni kuosha mchele wako.

3- Kisha injika tui jikoni weka chumvi na baadaye hiliki.

4- Hakikisha maji uliyoinjika yana uwezo wa kuivisha wali wako.

5- Baada ya kuiva palia na weka pembeni.



*KWA WALI WA RANGI YA CHUNGWA*

1- Anza kwa kupika wali wa mafuta. Kwa kuosha mchele na kuuchemsha kwa kiwango cha maji ya kutosha kuivisha.

2- Hakikisha unaweka chumvi ili kuufanya wali wako kuwa na ladha.

3- Chukua karoti na nyanya saga pamoja.

4- Kisha kaanga binzari na changanya na mchanganyiko wa nyanya na karoti.

5- Chukua wali wako uliokwishawiva na changanya katika mchanganyiko wako huo.


6- Wali wote utakuwa wa rangi ya chungwa.



*WALI WA KIJANI*

1- Kwa wali wa kijani , anza kwa kupika wali wenyewe kama nilivyoelekeza hapo juu.Kisha chukua kitunguu maji, saumu, tangawizi nazi , majani ya mnanaa,majani ya giligilani,hoho, pilipili manga na kisha saga kwenye machine ya kusagia.

2- Chukua mafuta ya kupikia weka jikoni, na kaanga garam masala na baadaye weka mchangayiko wako wa kijani kwenye sufuria hiyo iliyoko jikoni.

3- Endelea kukaanga hadi viive kabisa.

4- Ipua na changanya na wali wako. Utapata wali wa kijani.

Baada ya hapo pakua. Na weka kwenye bakuli lenye muundo unaopendelea.

5- Anza kwa kuweka rangi yeyote kati ya hizo ulizopika. Panga vizuri kwa kufuata mpangilio maalum unaweza kuanza na rangi ya machungwa, nyeupe na kijani ikaja mwisho au kinyume chake.

6- Pamba wali wako kwa kuweka jani dogo la giligilani na kipande cha karoti.

Chakula chako kipo tayari kwa kuliwa

*MTAMU BALAA*🤗🤗🤗

No comments:

Post a Comment