Monday, January 25, 2021

*JINSI YA KUPIKA EGGCHOP



*MAHITAJI*

1. Mayai yaliochemshwa 4.

2. Nyama ya kusaga robo kilo.

3. Kitunguu swaum.

4. Tangawizi.

5. Limao.

6. Chumvi.

7. Pilipili.

8. Breadcrambs.

9. Carry powder.

10. Binzari nyembamba ya unga.

11. Yai moja bichi.

12. Mafuta.
 

*JINSI YA KUANDAA*

🥕Marinate nyama na pilipili, kitunguu swaum, tangawizi, limao, chumvi, carry powder, binzari nyembamba na breadcrambs pamoja. 

🥕Kisha vunja yai moja bichi kwenye kibakuli na ulikoroge kisha tia kwenye mchanganyiko wa nyama.Gawanisha matonge manne kwa ajili ya kuzungushia kwenye mayai .

🥕Chemsha mayai kwa muda wa dakika 20. Yakisha iva acha yapoe na kisha yamenye maganda na uyaweke pembeni. 

🥕Baada ya hapo chukua yai moja lililochemshwa na ulizungushie donge moja la mchanganyiko wa nyama.

🥕 fanya hivyo kwa mayai yote yaliobakia. 

🥕Baada ya hapo paka mafuta kwa nje ya hizo eggchop na kisha paka mafuta kwenye sinia la kuokea na uziokee kwenye oven kwa moto wa kawaida, kwa muda wa dakika 20.Na eggchop zako zitakuwa tayari kwa kuliwa.

*Enjoy eggchop*🤗

*TAMU BALAA*🤗🤗🤗


*JINSI YA KUPIKA BAJIA ZA SAMAKI




*MAHITAJI:*

1. Samaki wa mnofu vipande 2, vikubwa.

2. Pilipili manga kijiko cha chai.

3. Maji ya ndimu kiasi.

4. Baking powder vijiko 2 vya chai.

5. Unga wa ngano kikombe 1.

6. Chumvi kiasi chako.

7. Kitunguu saumu kilichopondwa 1/2 kijiko cha chai.

8. Sukari 1/2 kijiko cha chai.

9. Kitunguu maji 1  kilichokatwa katwa.

10.  Majani ya kotmir yalokatwa katwa vijiko 2 vya chakula.

11. Hoho zilizokatwa katwa kijiko 1 cha chakula.

12. Yai 1.

13. Maziwa  ama maji 1/2 kikombe, utatia kdogo kidogo si lazima yatumike yote.


*NAMNA YA KUTAYARISHA NA KUPIKA BAJIA ZA SAMAKI:*


🧆Safisha samaki wako vizuri kisha mchemshe kidogo kwa chumvi, ndimu na pilipili manga. 

🧆Mnyambue samaki wako kupata chenga chenga unaweza mnyambua kwa mikono, blender au food processor. 

🧆 Changanya unga, baking powder 
 katika bakuli, ukishachanganya vizuri  tia mahitaji yalobaki isipokuwa maji/maziwa kisha changanya tena vizuri.

🧆 Anza kutia maji ama maziwa taratibu ukiwa wachanganya hadi kupata uzito mzuri wa kuchoteka kwa kijiko au mkono usiwe maji maji sana. 

🧆 Tia mafuta jikoni juu ya moto wa kiasi, yakipata moto chota mchanganyiko wako anza kuchoma.

*TAMU BALAA🤗🤗*




Sunday, January 24, 2021

*JINSI YA KUPIKA MIGUU YA KUKU



*MAHITAJI*

1. Miguu kiasi chako.

2. Ndimu/limau au ukwaju.

3. Mtindi (ukipenda).

4. Pilipili manga.

5. Manjano.

6. kitunguu swaum na tangawizi.

7. Majani ya iligilani.

8. Chumvi kiasi.

9. Pilipili.

10. Mafuta ya kupikia vijiko 3 vya chakula.

11. Nyanya 2 au 3 zilizosagwa.

12. Nyanya ya pakti 1(kufanya rojo liwe zito zaidi).


       *JINSI YA KUANDAA*

safisha vizuri miguu kisha weka kwenye chombo cha kupikia pamoja na hayo mahitaji yote, tia mafuta na maji kidg sana ya kuivishia tuu pika mpk iwive na ibaki na rojo kidogo iwe kavu isiwe na michuzi michuzi.

*Nb:*
🦴unaweza ukala na ugali, mikate, chipsi, chapati, ndizi choma au za kukaanga, wali n.k.

🦴kama miguu ni migumu unaweza kuichemsha kidogo kabla ya kupika kisha baadae utapikia na hio supu yake.

🦴pia unaweza ukatumia namna ya upishi kwenye utumbo,vichwa au firigisi.

*MITAMU BALAA*🤗🤗🤗.




Wednesday, January 20, 2021

JINSI YA KUPIKA MKATE WA KUMIMINA* 🍞🍞



                  *MAHITAJI

✓ Mchele Nusu kilo 
✓ Tui la nazi kikombe 1 -  2 
✓ Hamira kijiko 1
✓ Hiliki kiasi
✓ Ute wa Yai  1
✓ Sukari Robo  kikombe


        *NAMNA YA KUANDAA* 


➖Loweka mchele usiku 1 / Masaa 8

➖Saga kwenye blenda mchele,hamira,tui la nazi,hiliki hadi viwe laini..
➖Mimina sukari na ute wa yai kwenye mchanganyiko wako then changanya vizuri...kisha weka sehemu yenye joto uumuke

Weka sufuria jikoni mafuta kidogo yakipata moto mimina mchanganyiko wako

➖Baada ya dakika 5-10 mkate ukishaanza kushikana funika kwa ufuniko then weka kwenye oven moto 300° hadi uwive na kuwa rangi ya brown. Kama utatumia mkaa kadiria moto

➖Subiria mkate upoe ndipo uukate vipand vipande

➖Mkate wako yari kwa kuliwa 👏👏

*MKATE HUU MTAMU HATARI:* 🤗🤗

JINSI YA KUPIKA PALAUU LA NYAMA YA KUKU*


* MAHITAJI*

1. Mchele 1/2 kg(nusu kilo).

2. Kuku mmoja wa kiasi aliyekatwa katwa na kuoshwa vizuri.

3. Vitunguu maji 2 vilivyokatwa katwa slices.

4. Pilipili boga 1.

5. Karoti 1.

6. Dania 1.

7. Tomato/nyanya 2 zilizokatwa katwa au kublendiwa.

8. Viazi 3 vilivyokatwa katwa.

9. Tomato paste/nyanya ya mkebe vijiko 2 vya mezani.

10. Kitunguu thomu kijiko 1 cha mezani.

11. Kijiko 1 cha chai mdalasini iliopondwa.

12. Kijiko 1 cha chai pilipili manga iliopondwa.

13. Kijiko 1 cha chai bizari nyembamba iliopondwa.

14. Mafuta uto/mafuta ya kupikia takriban vijiko 3 vya mezani.

*JINSI YA KUANDAA*

🥕Marinate kuku (weka siki na chumvi kwenye kuku umuache kwa takriban nusu saa.

🥕Bandika sufuria motoni ueke mafuta, yakishika moto weka kitunguu ukikaange mpaka kiwe hudhurungi (golden brown).

🥕Weka spices zote(dawa za pilau) pamoja na kitunguu thomu upike kwa sekunde kadhaa.

🥕Weka tomato, pilipili boga , karoti ,tomato  paste na kuku ufunike uache ziive kwa takriban dakika 10.

🥕Weka mchele uupike kwa sekunde kadhaa
Weka viazi na maji kiasi. funika mpaka maji yaelekee kukauka, takriban dakika 10(kiasi cha maji itategemea na mchele.

🥕Mimi nimetumia sunrice kwa hiyo nimeweka maji kiasi cha kufunika mchele na kuzidi kidogo)
Weka dania ukoroge vizuri na uyaache maji yakauke vizuri.

🥕Kisha ufunike uweke moto mdogo kabisa kama unatumia gas cooker kwa takriban dakika 10_15(kama unatumia jiko la makaa weka moto wa juu na chini).

*Pilau ipo tayari*

🥕Andaa kwa  kachumbari , pilipili ya kukaanga na juice ya maembe.

*PILAU TAMU BALAA*🤗🤗🤗