*MAHITAJI:*
1. Samaki wa mnofu vipande 2, vikubwa.
2. Pilipili manga kijiko cha chai.
3. Maji ya ndimu kiasi.
4. Baking powder vijiko 2 vya chai.
5. Unga wa ngano kikombe 1.
6. Chumvi kiasi chako.
7. Kitunguu saumu kilichopondwa 1/2 kijiko cha chai.
8. Sukari 1/2 kijiko cha chai.
9. Kitunguu maji 1 kilichokatwa katwa.
10. Majani ya kotmir yalokatwa katwa vijiko 2 vya chakula.
11. Hoho zilizokatwa katwa kijiko 1 cha chakula.
12. Yai 1.
13. Maziwa ama maji 1/2 kikombe, utatia kdogo kidogo si lazima yatumike yote.
*NAMNA YA KUTAYARISHA NA KUPIKA BAJIA ZA SAMAKI:*
🧆Safisha samaki wako vizuri kisha mchemshe kidogo kwa chumvi, ndimu na pilipili manga.
🧆Mnyambue samaki wako kupata chenga chenga unaweza mnyambua kwa mikono, blender au food processor.
🧆 Changanya unga, baking powder
katika bakuli, ukishachanganya vizuri tia mahitaji yalobaki isipokuwa maji/maziwa kisha changanya tena vizuri.
🧆 Anza kutia maji ama maziwa taratibu ukiwa wachanganya hadi kupata uzito mzuri wa kuchoteka kwa kijiko au mkono usiwe maji maji sana.
🧆 Tia mafuta jikoni juu ya moto wa kiasi, yakipata moto chota mchanganyiko wako anza kuchoma.
*TAMU BALAA🤗🤗*
No comments:
Post a Comment