Sunday, January 24, 2021

*JINSI YA KUPIKA MIGUU YA KUKU



*MAHITAJI*

1. Miguu kiasi chako.

2. Ndimu/limau au ukwaju.

3. Mtindi (ukipenda).

4. Pilipili manga.

5. Manjano.

6. kitunguu swaum na tangawizi.

7. Majani ya iligilani.

8. Chumvi kiasi.

9. Pilipili.

10. Mafuta ya kupikia vijiko 3 vya chakula.

11. Nyanya 2 au 3 zilizosagwa.

12. Nyanya ya pakti 1(kufanya rojo liwe zito zaidi).


       *JINSI YA KUANDAA*

safisha vizuri miguu kisha weka kwenye chombo cha kupikia pamoja na hayo mahitaji yote, tia mafuta na maji kidg sana ya kuivishia tuu pika mpk iwive na ibaki na rojo kidogo iwe kavu isiwe na michuzi michuzi.

*Nb:*
🦴unaweza ukala na ugali, mikate, chipsi, chapati, ndizi choma au za kukaanga, wali n.k.

🦴kama miguu ni migumu unaweza kuichemsha kidogo kabla ya kupika kisha baadae utapikia na hio supu yake.

🦴pia unaweza ukatumia namna ya upishi kwenye utumbo,vichwa au firigisi.

*MITAMU BALAA*🤗🤗🤗.




No comments:

Post a Comment