*MAHITAJI*
✓ Mchele Nusu kilo
✓ Tui la nazi kikombe 1 - 2
✓ Hamira kijiko 1
✓ Hiliki kiasi
✓ Ute wa Yai 1
✓ Sukari Robo kikombe
*NAMNA YA KUANDAA*
➖Loweka mchele usiku 1 / Masaa 8
➖Saga kwenye blenda mchele,hamira,tui la nazi,hiliki hadi viwe laini..
➖Mimina sukari na ute wa yai kwenye mchanganyiko wako then changanya vizuri...kisha weka sehemu yenye joto uumuke
Weka sufuria jikoni mafuta kidogo yakipata moto mimina mchanganyiko wako
➖Baada ya dakika 5-10 mkate ukishaanza kushikana funika kwa ufuniko then weka kwenye oven moto 300° hadi uwive na kuwa rangi ya brown. Kama utatumia mkaa kadiria moto
➖Subiria mkate upoe ndipo uukate vipand vipande
➖Mkate wako yari kwa kuliwa 👏👏
*MKATE HUU MTAMU HATARI:* 🤗🤗
No comments:
Post a Comment