Wednesday, January 20, 2021

JINSI YA KUPIKA PALAUU LA NYAMA YA KUKU*


* MAHITAJI*

1. Mchele 1/2 kg(nusu kilo).

2. Kuku mmoja wa kiasi aliyekatwa katwa na kuoshwa vizuri.

3. Vitunguu maji 2 vilivyokatwa katwa slices.

4. Pilipili boga 1.

5. Karoti 1.

6. Dania 1.

7. Tomato/nyanya 2 zilizokatwa katwa au kublendiwa.

8. Viazi 3 vilivyokatwa katwa.

9. Tomato paste/nyanya ya mkebe vijiko 2 vya mezani.

10. Kitunguu thomu kijiko 1 cha mezani.

11. Kijiko 1 cha chai mdalasini iliopondwa.

12. Kijiko 1 cha chai pilipili manga iliopondwa.

13. Kijiko 1 cha chai bizari nyembamba iliopondwa.

14. Mafuta uto/mafuta ya kupikia takriban vijiko 3 vya mezani.

*JINSI YA KUANDAA*

🥕Marinate kuku (weka siki na chumvi kwenye kuku umuache kwa takriban nusu saa.

🥕Bandika sufuria motoni ueke mafuta, yakishika moto weka kitunguu ukikaange mpaka kiwe hudhurungi (golden brown).

🥕Weka spices zote(dawa za pilau) pamoja na kitunguu thomu upike kwa sekunde kadhaa.

🥕Weka tomato, pilipili boga , karoti ,tomato  paste na kuku ufunike uache ziive kwa takriban dakika 10.

🥕Weka mchele uupike kwa sekunde kadhaa
Weka viazi na maji kiasi. funika mpaka maji yaelekee kukauka, takriban dakika 10(kiasi cha maji itategemea na mchele.

🥕Mimi nimetumia sunrice kwa hiyo nimeweka maji kiasi cha kufunika mchele na kuzidi kidogo)
Weka dania ukoroge vizuri na uyaache maji yakauke vizuri.

🥕Kisha ufunike uweke moto mdogo kabisa kama unatumia gas cooker kwa takriban dakika 10_15(kama unatumia jiko la makaa weka moto wa juu na chini).

*Pilau ipo tayari*

🥕Andaa kwa  kachumbari , pilipili ya kukaanga na juice ya maembe.

*PILAU TAMU BALAA*🤗🤗🤗

No comments:

Post a Comment